Breaking

Monday, 4 August 2025

WANANCHI WAKARIBISHWA BANDA LA WIZARA YA NISHATI KUFAHAMU MIRADI INAYOENDELEA KUTEKELEZWA



Wizara ya Nishati imeendelea kukaribisha wananchi kutembelea Banda la Wizara ya Nishati katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima (NANENANE) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Fredrick Marwa, Mjiolojia kutoka Wizara ya Nishati amesema katika maonesho hayo Wizara inaeleza kuhusu kazi mbalimbal zinaoendelea kufanyika ikiwemo za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Bonde la Eyasi Wembere.


Marwa amesema wananchi watakapofika katika Banda la Wizara ya Nishati pia watajionea mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Wizara pamoja na Taasisi zake ikiwemo TANESCO, EWURA, REA na TPDC.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages