Breaking

Tuesday, 29 July 2025

MWENGE WA UHURU WAKOSHWA NA MIRADI YA MAENDELEO KALIUA



MKUU wa Wilaya ya Kaliua, Dk. Garald Mongela, amewaongoza maelfu ya wananchi wa wilaya hiyo kushiriki uzinduzi wa miradi ya kimkakati iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru.

Katika mwaka huu Mwenge wa Uhuru umezindua, umeweka mawe ya msingi na umetembelea miradi tisa ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi 2,275,516,058.60.

Miradi hiyo ni uzinduzi wa Klabu ya Wapinga Rushwa Shule yaSekondari Mwongozo, Ujenzi wa Nyumba ya Walimu ya Familia Mbili (Two in One) Shule ya Msingi Dk. Charles Msonde Shilingi 110,000,000 na Ujenzi wa Kitakasa Mikono Shule ya Msingi Dk. Charles Msonde Shilingi 10,205,313.

Miradi mingine ni Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) Zahanati ya Usigala Shilingi 72,400,000, Ujenzi wa Shule ya Sekondari Makingi

Shilingi 603,890,563 na Mtambo wa Kutengeneza Barabara (Motor Grader) Shilingi 1,227,000,000.

Miradi mingine iliyozinduliwa ni Barabara ya Kuelekea Kituo cha Afya Ulyankulu (km. 2) Shilingi 1,603,040.00, Mradi wa Maji Kijiji cha Ulindwanoni Shilingi 219,817,142.60 na Mradi wa Kikundi cha Bodaboda (Boma Road) Shilingi 30,600,000.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages