Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Samwel Shelukindo, alikutana na kufanya mazungumzo na Bw. Andrew Lentz, Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini.
Mazungumzo hayo, yaliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam, yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani katika maeneo ya maslahi ya pamoja.