Breaking

Wednesday, 6 April 2022

HAKUNA UHABA WA MAFUTA TANZANIA-WAZIRI MAKAMBA







Serikali kupitia Wizara ya Nishati imesema mpaka sasa Tanzania haina Uhaba wa Mafuta, hivyo hakuna Sababu ya Watanzania kuwa na Taharuki ya Ukosefu wa Nishati hiyo Muhimu.

Hayo yameelezwa leo Jumatano April 06, 2022 Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati, Januari Makamba katika mkutano wake na Waagizaji na Wasambazaji wa Mafuta hapa nchini.

Waziri Makamba amesema hakuna sababu kwa Wananchi kuwa na Taharuki ya Uhaba wa Mafuta kwa sababu bado ipo shehena ya kutosha ya Mafuta Kwenye Maghala yaliyopo na yale ambayo yanashushwa Bandarini.

"Hadi kufikia leo tunayo mafuta ya kutosha kutumika kwa takribani Siku 27, pia Serikali imeshaagiza mafuta yatayotumika Mwezi wa tano na wa sita ambayo yapo kwenye Mchakato," amesema Waziri wa Nishati January Makamba.


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) jana ilitangaza kuanza kutumika kwa bei mpya ya nishati hiyo ambapo kwa sasa Petroli itakuwa 2,861 kwa lita, Dizeli 2,692 na Mafuta ya taa 2,682 kwa lita.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages