Breaking

Wednesday, 4 March 2026

VIWANDA MKOANI PWANI VYATAKIWA KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo, akizungumza na menejimenti ya Kiwanda cha Keds Tanzania Co. Ltd kinachozalisha bidhaa mbalimbali za usafi katika ziara ya kikazi Mkoani Pwani.

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Rahma Kisuo, ameziagiza menejimenti za viwanda Mkoani Pwani kuboresha mazingira ya kazi namaslahi ya wafanyakazi ili kuwa na uzalishaji endelevu na wenye tija.

Ametoa agizo hilo katika ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa sheria mbalimbali za kazi ikiwemo Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 katikamaeneo mbalimbali ya kazi Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani.

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika viwanda vilivyotembelewa, Naibu Waziri Kisuoamesema pamoja na viwanda hivyo kufanya kazi nzuri ya uzalishaji na kutekelezasheria za kazi, ziara yake imabaini dosari ndogo ndogo zinazopaswa kurekebishwa nawahusika.

“Tumetembelea baadhi ya maeneo katika viwanda hivi na kujionea hali ilivyo. Kimsingiwanafanya vizuri japokuwa kuna kasoro chache tulizozibaini ikiwemo baadhi yawafanyakazi kutokuwa na mikataba ya ajira pamoja na kutokidhi baadhi ya viwango vyausalama na afya mahali pa kazi,” amesema Naibu Waziri Kisuo.

Amewaagiza watendaji kutoka Ofisi yake na Mamlaka nyingine za udhibiti, kutengamuda maalum wa kufanya ukaguzi wa kina katika viwanda hivyo ili kutoa ushauri stahikiwa maboresho yanayohitajika kwa wawekezaji.

Aidha, amewapongeza wamiliki wa viwanda husika kwa uzalishaji wenye mchangomkubwa katika uchumi wa nchi kupitia kodi inayolipwa serikalini pamoja na kuzalishaajira nyingi kwa Watanzania.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda, ambaye aliambatana na Naibu Waziri katika ziara hiyo, ameeleza baadhi yamapungufu yaliyobainika katika mifumo ya usalama na afya ya viwandavilivyotembelewa ikiwa ni pamoja na mazingira ya kazi yenye joto kali, vumbi la makaaya mawe kutapakaa katika mazingira, upungufu wa vifaa kinga na ukosefu wa alama za usalama.

Amemhakikishia Naibu Waziri kuwa watalaam wake watashirikiana na mamlakanyingine kufanya ukaguzi wa kina ambao utawezesha wawekezaji kupata ushauriunaohitajika ili kuboresha mazingira yao ya uzalishaji.

Kwa upande wao, viongozi wa viwanda vilivyotembelewa akiwemo Bw. Jacob Lerise, Msimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala katika Kiwanda cha uundaji magari cha GF Vehicle Assemblies Ltd, wamemshukuru Naibu Waziri na watendaji wake na kuahidikutekeleza maagizo mbalimbali yaliyotolewa katika ziara hiyo.

Ziara hiyo ya siku mbili Wilayani Kibaha Mkoani Pwani imefanyika katika kiwanda cha bidhaa za usafi cha Keds Tanzania Co. Ltd, Aluminium Trailers Ltd ambao ni waundajiwa trela za malori, kiwanda cha kuunda magari cha GF Vehicle Assemblies Ltd pamojakiwanda cha sabuni na vipodozi cha Creative Intertraders Ltd.


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo, akitembelea maeneo mbalimbali katika Kiwanda cha Aluminium Trailers Ltd wakati wa ziara yake ya kikazi aliyofanya Wilayani Kibaha Mkoani Pwani Machi 2-3, 2026. Alioambatana nao ni Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, Mkurugenziwa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma na Watendaji wenginekatika Ofisi ya Waziri Mkuu.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo, akiongea na wafanyakazi wa Kiwanda cha Aluminium Trailers Ltd wakati waziara yake ya kikazi aliyofanya katika Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani Machi 2-3, 2026. Alioambatana nao ni Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda na Watendajiwengine katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano).

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda na Watendaji wengine katika Ofisi yaWaziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) wakifuatilia maelekezo ya Naibu Waziri waNchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo (hayupopichani), wakati wa ziara yake ya kikazi aliyofanya katika Wilaya Kibaha Mkoani Pwani Machi 2-3, 2026.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo, akiangalia bidhaa zinazozalishwa na Kiwanda cha Aluminium Trailers Ltd wakatiwa ziara yake ya kikazi aliyofanya katika Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani Machi 2-3, 2026.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo, akiongea na wafanyakazi wa Kiwanda cha Aluminium Trailers Ltd wakati waziara yake ya kikazi aliyofanya katika Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani Machi 2-3, 2026. Alioambatana nao ni Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda na Watendajiwengine katika Ofisi ya Waziri Mkuu.

Wafanyakazi wa kiwanda cha bidhaa za usafi cha Keds Tanzania Co. Ltd wakimsikilizaNaibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo, wakati wa ziara yake ya kikazi aliyofanya katika Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani,Machi 2-3, 2026.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages