![]() |
| Mwandishi wa habari Samir Salum akikabidhiwa moja ya cheti na Mwanasheria wa bodi ya Ithibati Bi. Rehema Mpagama |
Dodoma, Tanzania
Mwanahabari Samir Salum amejizolea heshima kubwa baada ya kutunukiwa jumla ya vyeti vinne vya Recognition of Outstanding Achievement katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Dodoma (DOMECO) , baada ya kuhitimu elimu ya uandishi wa habari, utangazaji na mawasiliano kwa umma.
Samir ametambuliwa katika maeneo manne muhimu ya tasnia ya habari ikiwemo Mtayarishaji bora wa maudhui (Best Producer) , Ripota Bora (Best Reporter) , Msomaji bora wa habari (Best News Anchor) , na Best Graphics Designer, maeneo yanayoonyesha upeo mpana na uwezo wa kufanya kazi mbalimbali ndani ya sekta ya utangazaji.
Pia ametunukiwa cheti cha utambuzi wa kuwa kiongozi wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho akiwa kama msemaji Mkuu wa Serikali.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hizo, Samir alisema mafanikio hayo yamempa hamasa mpya ya kuendelea kufanya kazi kwa ubunifu na kuzingatia viwango vya juu vya kitaaluma.
Aidha, uthubutu na ubunifu wa Samir ndivyo vilivyompa nafasi ya kung’ara zaidi ya wanafunzi wengine.
Mafanikio hayo yanatarajiwa kufungua milango mipya kwa Samir katika vyombo vya habari ndani na nje ya nchi, huku akiahidi kuendelea kuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wanaosomea fani ya uandishi wa habari na utangazaji.
Uongozi wa Lango la habari unampongeza Samir Salum kwa kuhitimu na kutukiwa vyeti hivyo.
