Na Mwandishi wetu, Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kuwezesha wakulima kujikwamua kiuchumi kupitia mikopo yenye riba nafuu.
Ameyasema hayo leo Agosti 1, 2025 jijini Dodoma katika viwanja vya NaneNane alipotembelea Banda la TADB kabla ya kufungua rasmi maonesho hayo Kitaifa.
"Nawapongeza TADB na ninawaelekeza kuendelea kuwafikia watanzania wengi zaidi kwa ajili maendeleo endelevu ya nchi yetu, " alisisitiza Dkt Mpango
Akizungumza namna Benki hiyo inavyokuza uchumi amesema imewezesha vijana, akina mama kujiajiri kwa kupatiwa zana za kilimo zenye ubora na zenye kuleta tija.