
Mhandisi wa Mazingira na Miundombinu ya Maji kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),Mhandisi Boniphace Kyaruzi, aziungumza na Waandishi wa Habari.
.......
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limewahimiza Watanzania kuchukua hatua madhubuti za kulinda na kuhifadhi mazingira asilia, ili kuzuia uharibifu wa vyanzo vya maji kwa ajili ya ustahimilivu na uendelevu wa rasilimali maji, ambayo ni muhimu kwa maisha ya binaadamu, uchumi wa viwanda na kilimo pamoja na uhai wa viumbe vyote.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mhandisi wa Mazingira na Miundombinu ya Maji, Mhandisi Boniphace Kyaruzi, amesema kuwa mazingira ya vyanzo vya maji nchini yanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uharibifu wa uoto wa asili unaotokana na ukataji miti holela, kilimo ndani ya mita 60 kutoka kwenye vyanzo vya maji, uchafuzi wa vyanzo utokanao na matumizi mbolea za kisasa, shughuli za viwanda pamoja na utupaji holela wa taka za majumbani.
Ameeleza kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kuwa mazingira asilia ya vyanzo vya maji yanalindwa kwa lengo la kuhifadhi rasilimali hiyo muhimu kwa maisha ya binadamu na viumbe hai wengine.
Tunaweza kurejesha vyanzo vya maji vilivyopotea kwa kupanda miti na kurejesha uoto wa asili, pamoja na kudhibiti shughuli za kibinadamu katika maeneo ya vyanzo vya maji. Ni muhimu kuepuka kilimo ndani ya mita sitini kutoka kwenye vyanzo hivyo, kudhibiti taka za majumbani kwa kuzitupa katika maeneo rasmi, na kuhakikisha maji taka kutoka viwandani yanatibiwa kabla ya kutiririshwa,” amesema Mhandisi Kyaruzi.
Aidha, amewataka Watanzania kubadili mitazamo na tabia kuhusu usimamizi wa taka na uhifadhi wa mazingira ili kuepusha uchafuzi wa vyanzo vya maji, ambavyo ni msingi wa maisha kwa viumbe hai wote.
“Ni muhimu sana tutunze vyanzo vya maji. Maji ni uhai bila maji hatuwezi kupika, kunywa, kufanya usafi wala kuendesha shughuli za kiuchumi kama vile viwanda. Hata mazingira yenyewe hayawezi kustawi bila maji,” amesisitiza.
Mhandisi Kyaruzi amebainisha kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo vingi vya maji