Breaking

Wednesday, 6 April 2022

RAIS SAMIA AAGIZA KUKAMILISHWA KWA SHERIA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia na Habari kuhakikisha inakamilisha uandaaji wa sheria ya kulinda taarifa za Watu binafsi.


Agizo hilo amelotoa leo Jumatano April 06, 2022 Jijini Dodoma katika uzinduzi wa mfumo wa usafirishaji wa dharula kwa wanawake wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) unaotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Vodacom.


Amesema,kwa vile mfumo huo utahusisha ukusanyaji wa taarifa za watu binafsi unapaswa kuwa na usiri wa kipekee Ili kulinda faragha na kwamba sio taarifa zinakusnywa na kukutwa kwenye mitandao ya kijamii zinasambaa.


"Kwa vile mfumo huu utahusisha ukusanyaji wa taarifa mbalimbali za Watu naelekeza pia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuhakikisha inakamilisha uandaaji wa sheria ya kulinda taarifa za Watu binafsi, sio taarifa zimeshakusanywa Mama kachukuliwa taarifa zake tumbo lina sentimita ngapi, Mtoto yukoje tumboni taarifa hizo tunazikuta kwenye mitandao zinasambaa..... HAPANA, ile sheria ya kulinda taarifa za Watu naomba ikamilishwe" Amesema Rais Samia


Kwa upande wake, Waziri Nape Nnauye amesema wapo katika hatua za mwisho za mchakato wa kukamilisha utungaji wa Sheria hiyo ili kuongeza ulinzi na udhibiti wa taarifa zinazokusanywa kwenye mifumo mbalimbali.


Aidha Rais Samia ameongeza kuwa licha ya kuanzishwa kwa mfumo huo wa M-MAMA Serikali inahakikisha maeneo yote nchini yanakuwa na Gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) ambapo imeagiza magari hayo 233.


"Pamoja na mfumo huu wa M-MAMA serikaili imejitahidi kuhakikisha kwamba maeneo yetu yanakuwa na ambulance angalau kila kata ambulance Moja. Tumeagiza ambulance 233 kawaida, tumeagiza ambulance 25 advanced ambazo ni ngazi ya rufaa" Rais Samia


Ameongeza kuwa Serikali inatarajia kutoa ajira 32,000, baadhi ni kutoka sekta ya afya na elimu, ili kuboresha utoaji huduma za afya na elimu kwa wananchi.


“Tumejitahidi kuajiri watumishi katika Sekta ya Afya kwa mwaka jana watumishi 3600 na mwaka huu uchumi wetu umetoa nafasi ya ajira zipatazo 32,000 ndani ya Taifa letu kati ya hizo nyingi zitaenda kwenye sekta ya Afya na Elimu,” Rais Samia
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages