Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu Machi 14, 2022 amefanya uteuzi wa viongozi nane katika nyanja mbali mbali.
Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus imesema kuwa Rais Samia amemteua Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania Nchi ya Jamhuri ya Malawi ambapo awali alikuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.