Na Mwandishi Wetu
Kocha mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 28 ambacho kitaingia kambini kwaajili ya maandalizi ya mechi za kufuzu AFCON na CHAN pamoja na mechi mbili za kirafiki za kimataifa za kalenda ya FIFA.
Katika kikosi hicho alichokitangaza leo Jumanne Machi 15, 2022 mwalimu Poulsen amewajumuisha wachezaji wapya saba kwenye kikosi chake ambao ni Abutwalib Mshery(Yanga),Haji Mnoga (Weymouth-Uingereza)Abdulrazack Hamza (Namungo),Azizi Andambwile (Mbeya City) Ben Starkie(Spalding-Uingereza),George Mpole (Geita Gold) na Ibrahim Joshua(Tusker-Kenya).
"hatuwezi kuchukua wachezaji wote ,lakini tunatambua na kuwafatilia wachezaji wote na kambi hii ni maalumu kwa ajili ya kuwatazama wachezaji wapya kwa sababu tutakuwa na michezo minne kuanzia mwezi June,kama mnavyojua hakutakuwa na kalenda ya michezo ya kirafiki kwa mwezi April na May kwa hiyo kambi hii itatupa mwanya wa kuwaona wachezaji wapya ambao watatuonyesha kitu gani watatupa kwa ajili ya mashindano ya kufuzu kwa Afcon pamoja na Chan kwa Taifa Stars" amesema kocha Poulsen

![]() |
Majina ya wachezaji 28 walioitwa Taifa Stars |
Tanzania itacheza michezo miwili ya kirafiki kwenye kalenda ya michezo ya kimataifa dhidi ya timu za taifa za Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan mnamo tarehe 23 March na 29 March kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.