Breaking

Friday, 11 March 2022

MWANAFUNZI WA CHUO AKAMATWA AKIUZA MITIHANI YA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI



Na Samir Salum - Lango la habari 


Mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo cha Zetech cha Nchini Kenya, Oscar Brighton amekamatwa kwa makosa ya kukutwa na kuuza mitihani feki ya shule za Msingi na Sekondari za nchini humo.


Kulingana na Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) , mshukiwa huyo alikamatwa jana alhamisi Machi 10, 2022 na maajenti wa siri walio katika Baraza la Kitaifa la Mitihani la Kenya (KNEC) akiwa na mitihani hiyo ambayo alikuwa akiwauzia wanafunzi.

DCI imesema kuwa Brighton pia atuhumiwa kwa kuunda vikundi kadhaa vya Whatsapp ambapo wanafunzi ambao wanatarajia kuhitimu masomo yao walitakiwa kutoa pesa ili kupata mitihani hiyo.

Aidha, imeeleza kuwa Brighton alikuwa akiuza mitihani hiyo Sh1,600 za Kenya kwa masomo ya Jamii (tsh 32,400) hadi Sh2,600 za Kenya (tsh 52,700) kwa masomo ya Sayansi.

"Mshukiwa, ambaye ni mkosaji wa mfululizo kwa sasa yuko kizuizini, atashtakiwa kwa kukiuka kifungu cha 28 cha Sheria ya Makosa ya Mitihani ya Kitaifa nambari 29, 2012," DCI imeandika kupita mtandao wa kijamii wa Twitter.


Akizungumza  Jumatano Machi 09, 22 wakati wa kuhitimisha mtihani wa Shule za Msingi siku ya Jumatano, Waziri wa Elimu Prof George Magoha alitaja zoezi hilo kuwa suluhu la visa vichache vya udanganyifu.

Aliendelea kueleza kuwa wale wote waliohusika katika utovu wa nidhamu watakabiliwa na mkono kamili wa sheria, akiangazia kisa ambapo meneja wa kituo cha Marsabit alichukua picha ya karatasi ya mtihani na kuisambaza na wenzake.

Hapo awali, Waziri Mkuu alifichua kuwa usahihishaji katika karatasi kwa watahiniwa milioni 1.2 ulianza siku ya kwanza na matokeo yanapaswa kutoka baada ya wiki mbili. Ikiwa ndivyo, huu utakuwa mwaka wa pili wa matokeo ya shule za msingi kutolewa ndani ya wiki mbili baada ya kukamilika kwa majaribio hayo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages