Na Samir Salum
Leo Jumamosi Januari 10, 2026, wapenda sayansi ya anga wana fursa ya kipekee kushuhudia tukio maalum linaloitwa opposition of Jupiter, ambapo sayari hiyo kubwa zaidi katika mfumo wa Jua inaonekana kung’aa zaidi kuliko kawaida.
Tukio hili hutokea pale Dunia inapokuwa katikati ya Jua na Jupiter, hali inayofanya sayari hiyo ionekane karibu zaidi na Dunia.
Kutokana na hali hiyo, Jupiter inaonekana kubwa na ang’avu zaidi, na inaweza kuonekana kwa macho bila kutumia kifaa chochote maalum.
Sayari hiyo huonekana kuanzia jioni baada ya machweo na kubaki angani hadi alfajiri, hivyo kutoa muda wa kutosha kwa watazamaji wa anga kuifuatilia.
Kwa wale wenye darubini au binoculars, tukio hili linatoa nafasi ya kuona baadhi ya miezi mikubwa ya Jupiter kama Io, Europa, Ganymede na Callisto.
Wataalamu wa anga wanasema opposition ya Jupiter ni miongoni mwa nyakati bora zaidi za kuichunguza sayari hiyo kwa mwaka mzima.
