Waziri wa NchI Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu amekutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), leo Desemba 10, 2025, jijini Dodoma.
Mazungumzo hayo ni sehemu ya mwendelezo wa mikutano yake na Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo, ikiwa na lengo la kufahamu utekelezaji wa majukumu yao, kusikiliza changamoto, fursa na kutoa maelekezo ya kiutendaji yatakayoongeza ufanisi, uwajibikaji na tija katika utoaji wa huduma kwa wananchi.










