Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Namibia nchini, Mhe. Gabriel Sinimbo, katika tukio lililofanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma, Desemba 10, 2025
Katika mazungumzo yao, Mhe. Dkt. Maghembe amempongeza Mhe. Sinimbo kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo ya kuiwakilisha nchi yake hapa Tanzania na kumhakikishia ushirikiano kutoka Wizarani na Serikalini kwa ujumla wakati wote atakapokuwa akitekeleza majukumu yake ya Ubalozi hapa nchini.







