Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeendelea na juhudi zake za kuwawezesha wakulima kupitia mafunzo ya uelewa kuhusu huduma na bidhaa zake kwa wakulima 120 kutoka Wilaya za Songea Mjini, Songea Vijijini, Namtumbo pamoja na Madaba mkoani Ruvuma.
Mafunzo hayo yalifunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Brig. Gen. Ahmed Abbas Ahmed, ambaye aliwahimiza washiriki kutumia maarifa waliyopata kuboresha uzalishaji, kuongeza tija, na kuimarisha ufanisi katika shughuli zao za kilimo-biashara.
Miongoni mwa mada kuu zilizojadiliwa katika mafunzo hayo ni:
. Huduma na bidhaa za TADB
. Urasimishaji wa kilimo-biashara
. Mfuko wa Dhamana ya Mikopo kwa Wakulima Wadogo (SCGS)
. Hali ya kilimo, ufugaji na uvuvi katika Wilaya ya Songea Mjini
Uimarishaji wa vyama vya ushirika na AMCOS.
Washiriki wa mafunzo walihusisha:
1. Vikundi vya wakulima kutoka Nakaheguo Group, Nalima AMCOs, Lumbingu Farmers, Juhudi Mpitimbi Farmers, Luganga Farmers, Ngoni Organized Farmers Group, na Umatengo Farmers Group.
2. Wakulima binafsi kutoka maeneo ya Mtyangimbole, Mbinga Muhalule, Litisha, Nakahuga, Matomondo, Msamala, Namtumbo, na Mshangano.
3. Wajasiriamali wa Ruvuma Mwalu.








