Breaking

Tuesday, 4 November 2025

MR. BLACK ACHUKUA FOMU KUGOMBEA NAFASI YA SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA


Kijana kutoka Shinyanga Mjini, Peter Alex Frank, maarufu kwa jina la Mr. Black, amejitosa rasmi kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mr. Black amechukua na kurejesha fomu leo Novemba 4, 2025, katika Makao Makuu ya CCM Taifa, Dodoma, hatua inayomweka kwenye orodha ya watia nia wanaowania nafasi hiyo muhimu ya uongozi wa chombo cha kutunga sheria nchini.

Akiwa kijana pekee miongoni mwa watia nia waliorejesha fomu hadi sasa, Mr. Black amesema uamuzi wake unatokana na dhamira ya dhati ya kutumia uwezo alio nao katika kulinda na kusimamia kanuni, sheria na taratibu za Bunge, pamoja na kuhamasisha utendaji na uchapakazi wa wabunge katika majimbo yao.

“Nikiaminiwa na kupata nafasi hii, nitahakikisha Bunge linaendeshwa kwa weledi, hekima na mbinu za kisasa, likiwa chombo imara kinachowakilisha vyema maslahi mapana ya Taifa,” amesema Mr. Black mara baada ya kurejesha fomu.

Ameongeza kuwa anatambua ukubwa wa jukumu hilo na amewaomba Watanzania wote kumuombea ili adhima yake ya kulitumikia Taifa kupitia nafasi hiyo itimie.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages