Breaking

Tuesday, 11 November 2025

MHE MCHENGERWA AAPA KULITUMIKIA TAIFA


Na Yohana Kidaga- Dodoma

Bunge la 13 , Leo historia imeandika ukurasa mwingine wa heshima na uadilifu. Mbele ya Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Mohamed Mchengerwa ameapa kwa moyo wa uzalendo, uaminifu, na dhamira ya dhati ya kulitumikia Taifa.

Mikono juu, kitabu cha katiba mkononi, moyo ukiwa umejaa heshima kwa wananchi waliomwamini — ni ishara ya ujasiri na uwajibikaji. Sauti yake ilipoapa, haikuwa sauti ya mtu mmoja, bali sauti ya maelfu ya wananchi wa Rufiji waliomchagua kuwa mwakilishi wao, sauti ya matumaini, maendeleo na mabadiliko chanya.

Huu ni mwanzo wa safari nyingine ya utumishi, safari ya kuimarisha sauti ya wananchi bungeni, kusimamia haki, maendeleo na ustawi wa kila Mtanzania.

Katika kampeni zake Mhe. Mchengerwa alisisitiza kuendelea kufanya siasa za maendeleo katika jimbo lake na taifa kwa ujumla huku akiwataka wananchi kudumisha amani kwa maendeleo ya kizazi cha sasa na baadaye 

Mhe. Mchengerwa ni Mbunge wa tisa wa kuchaguliwa katika jimbo hilo la Rufiji toka lianzishwe na kuongozwa na wabunge kadhaa kuanzia Mhe. Bibi Titi Mohamed ambapo anaelezewa kuwa ni miongoni mwa wabunge walioliletea maendeleo makubwa Jimbo hilo ukilinganisha na wabunge waliotangulia.

Licha ya kuwa Mbunge wa tisa wa Jimbo hilo, Mhe. Mchengerwa ni miongoni mwa wanasiasa wachache nchini ambao wamehudumu kwenye mihimili yote katika nafasi za juu za uandamizi kwa mafanikio makubwa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages