Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa ameshiriki Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao kutokea jijini Dodoma Novemba 07, 2025.
Mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ni Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Mhe. Ronald Lamola alisema mkutano huo ni mwendelezo wa umoja wa nchi za SADC kuitana pamoja kujadili masuala mbalimbali yanayohitaji maamuzi ya haraka.
Mkutano huo umejadili maandalizi ya mkutano wa Daharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaofanyika kwa njia ya Mtandao jioni ya Novemba 07, 2025; masuala ya kibajeti ya ulinzi na usalama na uongozi wa SADC kufuatia kujitoa kwa Jamhuri ya Madagascar kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha August 2025-August 2026.








