Breaking

Friday, 5 September 2025

MAHOJIANO MAALUM NA ROSTAM AZIZ LEO SAA TATU USIKU AZAM TV

   


Mfanyabiashara na mwanasiasa maarufu kutoka Tanzania, Rostam Aziz, anatarajiwa kuzungumza leo kupitia Azam TV  (UTV) katika kipindi maalum cha mahojiano.


Kwa mujibu wa tangazo rasmi, mahojiano hayo yatafanyika leo Ijumaa, tarehe 5, Septemba 2025 kuanzia saa 3:00 usiku kupitia Runinga ya Azam.

Ingawa hakujatolewa dondoo rasmi za mada zitakazojadiliwa, mahojiano haya yanakuja katika kipindi ambacho hivi karibuni aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, amekuwa akimshambulia Rostam hadharani akimhusisha na tuhuma mbalimbali.

Watazamaji wanatarajiwa kufuatilia kwa karibu kusikia maoni na ufafanuzi wa Rostam kuhusu masuala ya kibiashara, kisiasa na mada moto zinazomhusu.

👉 Usikose kutazama Azam TV leo saa 3:00 usiku.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages