Breaking

Tuesday, 23 September 2025

KAMPENI ZA KATAMBI ZAPAMBA MOTO SHINYANGA MJINI

Wakazi wa Chibe wakiwa kwenye mkutano wa Kampeni
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Chibe - Picha na MALUNDE
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Chibe
Wakazi wa Chibe wakiwa kwenye mkutano wa Kampeni

Na Kadama Malunde – Shinyanga

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi, amesema mpango sahihi wa maendeleo kwa wananchi ni sera na ilani ya CCM ambayo imejidhihirisha katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kijamii na kiuchumi ndani ya jimbo hilo na taifa kwa ujumla.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Jumanne Septemba 23, 2025, katika kata ya Chibe, Katambi amewaomba wananchi kumpa ridhaa ya kuendelea kuwa Mbunge wao ili aendelee kutatua changamoto na kuwaletea maendeleo zaidi.

“Mpango sahihi wa maendeleo ni CCM. Tumedhamiria kuendelea kuboresha maisha ya wananchi katika sekta zote ikiwemo elimu, afya na maji. Katika miaka mitano tumefanikisha miradi mikubwa, tunaomba kura zenu ili tuendelee kusonga mbele,” amesema Katambi.

Amefafanua kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita amefanikisha miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi, hususan katika sekta za elimu, afya, maji na barabara. 

Hata hivyo, amebainisha kuwa bado kuna changamoto zinazohitaji kushughulikiwa, hivyo akawaomba wananchi wampe ridhaa nyingine ili kuendelea kuzipatia majibu changamoto hizo.

Aidha, amewahimiza wananchi kumpigia kura nyingi za ushindi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wote wa CCM, akisisitiza kuwa chama hicho ndicho chenye dira ya kweli ya maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Wazazi CCM Taifa, Edwin Peter Nyakanyenge, amewataka wanachama na wapenzi wa CCM kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa wagombea wote wa chama hicho.

“Sasa hivi kazi tuliyonayo ni moja tu, ni kutafuta kura za CCM. Tuhakikishe Dkt. Samia anaongoza kura, Mbunge Katambi anaongoza kura na madiwani wote wa CCM wanaongoza kura. Tutembee kifua mbele kwa sababu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita yako dhahiri – afya mnaona, shule mnaona, maji mnaona, umeme mnaona. Tutashindwaje kushinda? Tutashinda kwa kishindo,” amesema Nyakanyenge.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa wanachama wa CCM kuendelea na mikakati ya ndani kwa kushirikiana na makundi mbalimbali ya kijamii badala ya kutegemea mikutano ya hadhara pekee.

Naye Mgombea Udiwani Kata ya Chibe, Peter Kisandu, amewahimiza wananchi kuipigia kura CCM akisisitiza kuwa chama hicho kimejipanga kuimarisha huduma za afya, barabara na upatikanaji wa maji safi na salama katika kata hiyo na maeneo mengine ya manispaa.

ANGALIA PICHA
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Chibe
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Chibe
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Chibe
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Chibe
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Chibe
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Chibe
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Chibe
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akinadi sera za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Chibe, kulia ni Mgombea Udiwani Kata ya Chibe, Peter Kisandu
Mgombea Udiwani Kata ya Chibe, Peter Kisandu akinadi sera za CCM

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Wazazi CCM Taifa, Edwin Peter Nyakanyenge akinadi wagombea wa CCM ( Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ubunge - Patrobas Katambi na Madiwani wa CCM) wakati wa mkutano wa kampeni za Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini uliofanyika katika kata ya Chibe.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anord Makombe akinadi sera za CCM

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Wazazi CCM Taifa, Edwin Peter Nyakanyenge akizungumza na wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini na kuwapa maelekezo ya kimkakati kuhusu kampeni na uchaguzi.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza kwenye kikao hicho
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Kibabi akizungumza kwenye kikao hicho

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages