Breaking

Thursday, 7 August 2025

WMA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA VIPIMO KWA WANAFUNZI




Na Okuly Julius, OKULY BLOG, DODOMA


Wanafunzi wa Shule ya Msingi Brother Martin ya mkoani Dodoma wamepata elimu ya vipimo kutoka kwa Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Wakala wa Vipimo (WMA), Veronica Simba, walipotembelea Banda la Wakala huo katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye Viwanja vya Nanenane, Nzuguni jijini Dodoma.

Moja ya mikakati ya Wakala wa Vipimo katika kupanua wigo wa utoaji elimu hiyo ni kuanzisha vilabu vya vipimo katika shule mbalimbali nchini ili kuwajengea wanafunzi uelewa wa masuala ya vipimo tangu wakiwa wadogo.









Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages