Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Kisaka Meena ametembelea banda jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu leo Agosti 2, 2025 katika maonesho ya Wakulima ya Nanenane.
Akizungumza wakati wa kutembelea banda hilo, ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zake kwa elimu inayoendelea kutoa kwa umma na wadau katika maonesho hayo.