Breaking

Wednesday, 13 August 2025

MFANYABIASHARA MAARUFU ARUSHA NATHAN KIMARO AICHANGIA CCM MILIONI 20 KUFANIKISHA KAMPENI UCHAGUZI MKUU


Na Mwandishi Wetu

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mfanyabiashara maarufu jijini Arusha,Nathan Kimaro ametoa Sh.milioni 20 kama sehemu ya mchango wake wa kusaidia kampeni za Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

Kimaro mbali ya kuchangia lakini pia alikuwepo ukumbini hapo jana Agosti 12,2025, kushuhudia ‘LIVE’ hafla hiyo ya Harambee ikiendelea ndani ya ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.

Harambee hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa Chama Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan,ikilenga kukusanya kiasi cha fedha shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya Kampeni za uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Aidha katika harambee hiyo,Chama cha Mapinduzi (CCM) kilifanikiwa kuchangisha kiasi cha fedha, jumla ya shilingi Bilioni 86.31 zikiwemo na ahadi,ambapo kuchangia huko kutafika tamati Agosti 27,2025 .

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages