Tanzania na Japan zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara, uwekezaji, uendelezaji rasilimali watu, miradi mikubwa ya maendeleo na miradi ya msingi (Grassroots projects), na kilimo ikiwemo ukuzaji wa uzalishaji wa mazao ya kahawa, pamba na korosho.
Hayo yamebainishwa wakati wa kikao kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mheshimiwa Takeshi Iwaya kilichofanyika pembezoni mwa Mkutano wa TICAD 9 jijini Yokohama Agosti 21, 2025.