Timu ya Kitaifa ya Wataalam ya kuandaa Mpango wa Pili wa Maboresho ya Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI II) ipo mkoani Mwanza kupata maoni ya wadau kuhusu changamoto zinazokwamisha biashara na uwekezaji nchini.
Lengo ni kupata taarifa zitakazosaidia kuandaa MKUMBI II. Utekelezaji wa MKUMBI II unatarajiwa kuongeza kasi katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuleta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali ambazo zitaibuliwa na sekta binafsi.