Breaking

Wednesday, 16 July 2025

MJUMBE WA INEC MHE. RWEBANGIRA ATEMBELEA MAFUNZO YA WATENDAJI WA UCHAGUZI TABORA NA KIGOMA

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Magdalena Rwebangira, leo Julai 16,2025, ametembelea mafunzo yanayofanyika kwa Watendaji wa Uchaguzi ngazi ya Mkoa na Jimbo kwa Mkoa wa Tabora na Kigoma yanayoendelea katika kituo cha Tabora.

Mjumbe Mhe.Rwebangira ameshuhudia mada mbalimbali zikiendelea kuwasilishwa sambamba na mafunzo yanayofanyika kwa njia ya vitendo.

Mafunzo haya ya siku tatu yamejumuisha Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa, Wasimamizia wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi na Maafisa Ununuzi, yanaendelea ikiwa ni siku ya pili huku yakitarajia kutamatika tarehe 17 Julai, 2025.

#KuraYakoHakiYakoJitokezeKupigaKura:
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages