
Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imewapiga marufuku watangazaji wa kituo cha redio cha Mjini FM kujihusisha na kazi za kihabari kuanzia Julai 18, 2025, kufuatia ukiukwaji wa Sheria na maadili ya taaluma ya habari.
Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi hiyo, adhabu hiyo inawahusu watangazaji Deodatha William, Mussa Crispin Mgenge, Perfect Crispin na Iddy Bakari Iddy waliokuwa wakirusha kipindi mubashara kiitwacho GENGE LA GEN TOK, kilichofanyika Julai 16, 2025 ambapo walifanya mahojiano na msanii wa Singeli aitwaye Dogo PATEN.
