
Maafisa wa wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wakiendelea kutoa elimu, ufafanuzi na utatuzi wa changamoto mbalimbali za urasimishaji , katika Ofisi za BRELA Makao Makuu, zilizopo katika makutano ya mtaa wa Shaban Robert na barabara ya Sokoine Jijini Dar es salaam. Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yalianza tarehe 16 Juni, 2022 na yatahitishwa rasmi tarehe 23 Juni, 2022. Nyote mnakaribishwa.




 
 
 
 
 
 
 
 
 
