Na Mwandishi Wetu-Lindi
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watendaji wa kata na vijiji nchini kusimamia vyema utawala bora na utawala wa sheria ikiwa ni pamoja na kuimarisha mfumo wa utatuzi wa migogoro sambamba na ushirikishaji wananchi katika maamuzi na mipango ya maendeleo.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo Alhamisi, Aprili 14, 2022 wakati akifungua mafunzo ya utawala bora kwa Watendaji wa Kata na Vijiji wilayani Ruangwa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Hanns Seide.
Waziri Mkuu amesema kuwa Uwazi ni moja ya msingi wa utawala bora hivyo kuwataka viongozi hao kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za utekelezaji wa mipango na bajeti zake.
"Toeni taarifa za mapato na matumizi. Hii itaondoa hisia za uwepo wa ubadhirifu na mtajenga imani kwa wananchi.”
“Nendeni mkatambue makundi yote katika jamii ili kila mwananchi atambue nafasi yake ya kuwa yeye ni sehemu ya jamii na pia ana mchango na haki ya kupata maslahi. Utatuzi wa migogoro katika maeneo yenu ya utendaji uwe kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.”
Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka watendaji hao wahamasishe umuhimu wa mbio za mwenge kama moja ya alama za nchi yetu. “Wananchi wafahamishwe historia ya mwenge ili waweze kuuthamini kama njia moja ya kumuenzi Baba wa Taifa letu.”
“Sote tunafahamu mbio za mwenge pamoja na mambo mengine zimekuwa zikitumika kukagua miradi inayotekelezwa katika halmashauri na kuweka mawe ya msingi katika baadhi ya miradi. Tuwaelimishe wananchi wasikubali kushawishiwa kuipinga historia ya Taifa letu.”