
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, ameshiriki ibada ya kitaifa ya kuaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Uganda, Mhe. Jacob Oulanyah katika Viwanja vya Kololo, Jijini Kampala nchini Uganda.

Marehemu Jacob alifariki dunia Machi 20, 2022 nchini Marekani, alipokuwa akipatiwa matibabu.

