Breaking

Sunday, 13 March 2022

MAHER ZAIN ATUNUKIWA ZAWADI NA WAZIRI MCHENGERWA..APENDEZWA NA VIVUTIO VYA TANZANIA

Na Mwandishi Wetu 


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mohamed Mchengerwa  amemkabidhi zawadi ya mfano wa meli mwanamuziki maarufu Duniani mwenye asili ya Lebanoni Maher Zain kutoka nchini Sweden anayejulikana kwa Nyimbo za Nasheed, kama sehemu ya kuhamasisha utalii hapa nchini.

Waziri Mchengerwa amemkabidhi zawadi hiyo katika tamasha la siku moja lililofanyika usiku wa Machi 12 jijini Dar es Salaam, maalum kwa ajili ya kuwezesha ununuzi wa vyombo vya usafiri na kukuza kipato kwa walemavu wasio ona wanaolelewa katika kituo cha Vimdat kilichoko Kisemvule jijini Dar es Salaam.



Akizungumza na mamia ya mashabiki wake waliofurika kuburidika na nyimbo zake kabla ya kuhitimisha tamasha hilo, mwanamuziki huyo maarufu wa Nasheed duniani aliyevalia tisheti yenye maneno (Tanzania Unforgettable) amesema uwepo wake Tanzania ni jambo asiloweza kulisahau maishani mwake kutokana na uzuri wa Tanzania na ukarimu wa watu wake.

“Naishukuru Serikali ya Tanzania na ninakupongeza Mheshimiwa Waziri kukuona hapa na wewe umekuja kuburudika na nyimbo zangu kweli Tanzania siyo ya kusahulika” alisema Maher



Akizungumza kwa niaba ya waandaji wa tamasha hilo Mwenyekiti msaidizi Yousra Alnahd amesema tamasha hilo lililopewa jina la Maher Zain in Tanzania pamoja na mapato ya tamasha hilo kulenga ununuzi wa vyombo vya usafiri kwa ajili ya kituo hicho, pia waandaji walilenga kuitangaza utalii kama sehemu ya kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu katika kuitangaza Tanzania na vivutio vyake. 

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages