Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Seleman Jaffo ameunda timu maalum itakayochunguza chanzo cha mabadiliko katika mto Mara yaliyopelekea maji kubadilika kuwa meusi huku viumbe hai wakiwepo samaki kufa.
Waziri Jafo ameunda kamati hiyo leo Jumamosi Machi 12, 2022 muda mchache baada ya kufika katika mto huo kujionea hali halisi hali iliyopeleka kuundwa kwa timu hiyo na kuitaka ifanye uchunguzi huo ndani ya siku saba kuanzia leo March 12, 2022 na kuiwasilisha kwake March 19, 2022.
Awali Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria (LVBWB) imeeleza kuwa uchunguzi wa awali wa kimaabara umebaini uwepo wa kiwango kikubwa cha mafuta na kukosekana kwa hewa ya Oksijeni kwenye maji ya mto Mara jambo lililosababisha samaki na viumbemaji kufa.
Tazama hapa chini majina ya Kamati iliyoteuliwa
