; //]]>
  • Home
  • About
  • Contact

LANGO LA HABARI
    • HABARI
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • MATUKIO
    • MAGAZETI
    • MADINI
    • MICHEZO
    • BURUDANI
    • MAKALA
  • Breaking

    Thursday, 24 March 2022

    Home HABARI KITAIFA WAZIRI BITEKO AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI WIZARA YA MADINI, AWATAKA KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA RUSHWA

    WAZIRI BITEKO AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI WIZARA YA MADINI, AWATAKA KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA RUSHWA

    Lango la Habari March 24, 2022 ,HABARI ,KITAIFA




    WAZIRI wa Madini, Dkt.Doto Biteko amezindua Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Madini huku akiwapongeza kwa namna ambavyo wanafanya kazi kwa ufanisi, hivyo kuwezesha mafanikio chanya nchini.


    Waziri Dkt. Biteko amezindua baraza hilo jana jumatano Machi 23, 2022 mkoani Morogoro huku akirejea wito wake wa mara kwa mara kwa watumishi kuwa, wanapaswa kufanya kazi kwa uadilifu na kuepuka vitendo vya rushwa.

    Amesema, Sekta ya Madini ni moja ya sekta ambayo inatakuwa kuwa makini na vitendo vya rushwa kwani inadhoofisha utoaji huduma na kuondoa haki kwa wananchi.

    "Wizara haitamvumilia mtumishi yoyote atakayebainika na kuthibitika kujihusisha na vitendo vya rushwa. Hakikisheni mnabeba dhamana hii na kutekeleza kikamilifu wajibu wenu kwa weledi na kwa kuzingatia maadili ya kitaaluma na ya utumishi wa umma,"amesema Waziri Dkt Biteko


    Aidha amewaasa kujadili namna ya kuimarisha ustawi wa wafanyakazi na kujifanyia tathmini kuelekea miaka mitano tangu kuanzishwa kwa wizara hiyo.


    "Nendeni mkawakumbushe watumishi mnaowaongoza hivi karibuni wizara inatimiza miaka 5 tangu kuanzishwa kwake, jifanyieni tathmini msibweteke na mafanikio yaliyopatikana, angalieni viashiria hatarishi mvifanyie kazi msirudi nyuma" amesema



    Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adolf Ndunguru amsema kuwa, umoja, mshikamano na bidii za watumishi hao zimewezesha kukusanya Shilingi Bilioni 406 kuanzia Julai 2021 hadi Februari 2022.


    Amesema mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa umeendelea kuimarika. 

    "Katika kipindi hiki mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa umendelea kuimarika ambapo katika kipindi cha miezi tisa (Januari hadi Septemba 2021) mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la taifa uliongezeka hadi kufikia asilimia 7.3 kutoka mchango wa asilimia 6.5 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2020.



    "Katika robo ya Tatu Julai- Septemba 2021, Sekta ya Madini imechangia asilimia 7.9 ya Pato la Taifa, Mwelekeo unaonesha kuwa malengo yetu ya kuhakikisha sekta hii inachangia asilimia 10 ya Pato la Taifa ifikapo mwaka 2025 kama ilivyo matakwa ya Dira ya Taifa ya Maendeleo, 2025 na Mpango wa tatu wa Maendeleo ya Taifa yanatekelezeka kila mtu akitimiza wajibu wake.


    "Katika kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi kufikia Februari 2022, tumefanikiwa kukusanya maduhuli ya shilingi bilioni 404.6, sawa na asilimia 62.6 ya lengo la makusanyo.


    Amefafanua kuwa, kupitia STAMICO imewezesha mafunzo na huduma mbalimbali kwa wachimbaji wadogo wapatao 1,144 waliotembelea vituo vya mfano vya Katente, Lwamgasa na Itumbi.


    "Tumendelea kutangaza fursa zilizopo katika Sekta ya Madini kupitia mikutano ya kitaifa, kikanda na kimataifa ukiwemo mkutano wa kimataifa tulioandaa mwezi februari 2022. Tumeboresha Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali kwa lengo la kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji.


    Pamoja na mafanikio Katibu Ndungulu amesema wizara hiyo inakabiliwa na changamoto za uwepo wa shughuli za utoroshaji wa madini zinazosababisha upotevu wa mapato ya serikali, uelewa mdogo wa wachimbaji, wafanya biashara wa madini na umma kwa ujumla kuhusu Sheria ya madini, hivyo kusababisha uwepo wa migogoro ya mara kwa mara.


    "ili kukabiliana na changamoto hizo,amesema wizara imeweka mikakati na hatua mbalimbali ya kukabiliana nazo ikiwemo kuimarisha usimamizi wa shughuli za madini na ukusanyaji wa mapato ya serikali yatokanayo na wasilimali madini kwa kushirikisha mamlaka mbalimbali." Ameeleza 




    Naye Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara ya Madini, Joseph Ngulumwa amesema kuwa, wanaushukuru uongozi wa wizara kwa namna ambavyo wamekuwa wakiwezesha watumishi kuhudhuria mafunzo mbalimbali.


    "TUGHE tunatoa shukrani za dhati kwa uongozi wa wizara kwa kuendelea kuwezesha watumishi kuhudhuria mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwani mafunzo haya yanasaidia kuongeza weledi na ufanisi katika kazi za wizara."Katika kuongeza uwezo wa watumishi, tunashauri watumishi kupatiwa uzoefu katika nchi zilizoendelea katika shughuli za uchimbaji madini na utafiti wa madini kama Australia, Canada na mataifa mengine yaliyoendelea. Aidha, tunashauri kuweka bajeti ya kusomesha wataalam nje ya nchi katika Shahada za Uzamili na Uzamivu walau watumishi 5 kwa mwaka.


    "TUGHE inatambua kuwa michezo ni sehemu ya kuboresha afya kwa watumishi hivyo, Uongozi wa TUGHE unashauri wizara kuwezesha watumishi kushiriki michezo mbalimbali mfano SHIMIWI na BONANZA kwa kuwa na bajeti ya kutosha na kushiriki vema.
    "Kwa niaba ya wafanyakazi, tunaomba suala la wafanyakazi bora kuongeza idadi kutoka mtumishi mmoja kuwa watumishi wawili kwa kila Idara na Kitengo ili kupanua wigo wa motisha kwa watumishi,"amesema Mwenyekiti huyo.










    TAZAMA MATUKIO YA PICHA HAPA CHINI
























    Tags HABARI# KITAIFA#
    Share This
    Author Image

    About Lango la Habari

    KITAIFA
    by Lango la Habari - March 24, 2022
    Tags HABARI, KITAIFA
    Newer Post Older Post Home
    Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990
    Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

    LANGO LA HABARI TV

    ZILIZOKIKI WIKI HII

    • DKT.SWARE SEMESI- NEMC ASHIRIKI UZINDUZI WA MFUMO W KIDIGITALI NCHINI GHANA
      NEMC imeshiriki uzinduzi wa mfumo wa kidigitali wa kufuatilia uchafuzi wa mazingira(online continuous emissions monitoring System) ambao um...
    • SHINCHEONJI TAEKWONDO TEAM WINS MEDALS AGAIN IN INTERNATIONAL COMPETITION, ELEVATING GLOBAL STATUS
      SHINCHEONJI TAEKWONDO TEAM WINS MEDALS AGAIN IN INTERNATIONAL COMPETITION, ELEVATING GLOBAL STATUS
        The Shincheonji Taekwondo Team poses for a commemorative photo at the ‘2025 Park Jung-hee Cup International Open Taekwondo Championships.’...
    • OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI YATOA HUDUMA MAONESHO NANENANE
      OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI YATOA HUDUMA MAONESHO NANENANE
    • SHILINGI TRILIONI 1.2 ZA BARRICK NA TWIGA KIBINDONI KWA WAZABUNI WAZAWA WA KITANZANIA
      SHILINGI TRILIONI 1.2 ZA BARRICK NA TWIGA KIBINDONI KWA WAZABUNI WAZAWA WA KITANZANIA
        Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick Mining Corporation Mark Bristow 👉Sera ya Maudhui ya ndani ikitumika katika sekta zote itachochea u...
    • CARMATEC YATOA MAFUNZO YA UTENGENEZAJI WA MAJIKO YA NISHATI SAFI KWA MAAFISA MAGEREZA.
      CARMATEC YATOA MAFUNZO YA UTENGENEZAJI WA MAJIKO YA NISHATI SAFI KWA MAAFISA MAGEREZA.
      Na Ferdinand Shayo ,Arusha . Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kimetoa mafunzo ya utengenezaji wa majiko ya nishati...
    • KALIUA YANUNUA MTAMBO WA KUTENGENEZA BARABARA
      KATIKA kutekeleza mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan wa kuhakikisha barabara za mijini na vi...
    • MWENGE WA UHURU WAKOSHWA NA MIRADI YA MAENDELEO KALIUA
      MKUU wa Wilaya ya Kaliua, Dk. Garald Mongela, amewaongoza maelfu ya wananchi wa wilaya hiyo kushiriki uzinduzi wa miradi ya kimkakati iliyo...
    • TAZAMA HAPA MATOKEO YA MTIHANI WA UALIMU DSEE, GATCE, GATSCCE 2025 NA KIDATO CHA SITA ACSEE 2025
      TAZAMA HAPA MATOKEO YA MTIHANI WA UALIMU DSEE, GATCE, GATSCCE 2025 NA KIDATO CHA SITA ACSEE 2025
        TAZAMA MATOKEO HAPA GUSA HAPA KUTAZAMA MATOKEO  YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA (ACSEE) 2025 GUSA HAPA KUTAZAMA MATOKEO  YA MTIHANI WA UALIM...
    • Oryx Yatoa Vibanda vya Kisasa kwa Askari, Yaahidi Elimu kwa Madereva Nchini
      Oryx Yatoa Vibanda vya Kisasa kwa Askari, Yaahidi Elimu kwa Madereva Nchini
      Kampeni ya kitaifa ya Chuma kwa Chuma Sio Poa, yenye lengo la kuhamasisha usalama barabarani, imezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam kw...
    • BIL 36.596 ZA MRADI WA SEQUIP ZILIVYO INUFAISHA DODOMA KWENYE SEKTA YA ELIMU
      BIL 36.596 ZA MRADI WA SEQUIP ZILIVYO INUFAISHA DODOMA KWENYE SEKTA YA ELIMU
      Mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa maeneo ambayo yamepata fedha nyingi kupitia mradi wa kuimarisha ubora wa Elimu ya sekondari nchini SEQUIP amb...

    MICHEZO

    Categories

    BURUDANI HABARI HALI YA HEWA KITAIFA MAGAZETI MAHUSIANO

    Pages

    WASILIANA NASI

    Name

    Email *

    Message *

    KUHUSU SISI

    Lango la Habari ni tovuti inayojihusisha na usambazaji wa taarifa mbalimbali katika nyanja za kitaifa, kimataifa, biashara, michezo na burudani.

    Tags

    HABARI KITAIFA MAGAZETI MATUKIO MICHEZO DAWASA MADINI LIVE BURUDANI KIMATAIFA UTEUZI African Doctors ZOOM BRELA AJIRA MAHUSIANO BIASHARA MAKALA KENYA CHADEMA LOLIONDO MITIHANI UKATILI SAMIR SIASA TZ-MW MONKEYPOX TRENI HALI YA HEWA UTAMADUNI MAPENZI haba ki

    Send Quick Message

    Name

    Email *

    Message *

    Copyright © LANGO LA HABARI