Breaking

Saturday, 12 March 2022

WASANII ZAIDI YA 200 WAKUTANISHWA, KUTUMBUIZA SERENGETI MUSIC FESTIVAL 2022



Wasanii zaidi ya 200 wanaotarajia kutumbuiza kwenye Tamasha kubwa la Muziki la Serengeti wameshiriki usiku wa  chakula  cha pamoja uliowakutanisha na viongozi mbalimbali wa Serikali.


 Katika usiku huo wa chakula cha pamoja wasanii hao wamekutana na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemimo Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kamishna wa Sensa  nchini Anna  Makinda.


Warsha hiyo ya chakula cha jioni iliyofanyika usiku wa leo Ijumaa Machi 11, 2022 imewapa fursa wasanii  kuelimisha  umuhimu wa sensa.

Wasanii hao wakiongozwa na Bushoke wamekonga nyoyo za  wa wageni mbalimbali walioshiriki  usiku huu.


Mbali na  viongozi Wakuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo,wageni wengine ni wabunge na wakuu wa taasisi mbalimbali za fedha na binafsi na watu mashughuli.


Aidha, wasanii wamepata nafasi ya kubadilishana mawazo na viongozi mbalimbali wa makampuni walioshiriki huku Mdhamini Mkuu wa shughuli hii akiwa ni Bank ya CRDB.


Tamasha la Muziki la Serengeti litalofanyika jijini Dodoma Kesho Jumamosi Machi 12 na Jumapili Machi 13, 2022 ikiwa ni mwaka mmoja toka kuingia madarakani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. 

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages