Tukio la kusikitisha limetokea nchini Marekani baada ya mtoto wa miaka mitatu kumuua mama yake kwa kumpiga risasi shingoni.
Mkuu wa Polisi wa Dolton nchini marekani, Robert Collins amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa limetokea siku ya Jumamosi Machi 12, 2022 majira ya saa usiku katika mji wa Dolton ambapo mama wa mtoto Daejah Bennett (22) na Romell Watson (23) walikuwa njiani kwenye gari wakielekea katika manunuzi wakati mtoto wao wa miaka mitatu alikuwa amekaa kiti cha nyuma.
Collins amesema kuwa mtoto huyo alichukua bastola aliyoipata kwenye kiti hicho na kufyatua risasi ambayo ilipelekea kifo cha mama ake Daejah Bennett mwenye umri wa miaka 22.
"Kwa namna fulani alishika bunduki na kuanza kucheza nayo, akaelekeza bunduki upande wa ma ake na kufyatua risasi iliyompiga mama ake shingoni" Collins alisema.
Daejah alikimbizwa hospitali ya Chuo Kikuu cha Chicago lakini alipoteza maisha muda mfupi tu baada ya kufikishwa hospitalini hapo.
Tukio hilo limeacha maswali mengi nchini Marekani huku baba wa mtoto Romell Watson (23) alikamatwa na polisi na kuachiwa Jumatatu Machi 14, 2022 ambapo tayari uchunguzi umeanza kuhusiana na umiliki wa silaha hiyo kama ulikuwa ni kwa njia ya halali au la.
Maelfu ya raia wa Marekani huuawa kila mwaka katika matukio ya mashambulizi ya silaha za moto katika maeneo tofauti ya nchi hiyo.
Kulingana na kikundi cha utetezi wa udhibiti wa umiliki wa bunduki, Everytown for Gun Safety, kimeeleza kuwa mnamo mwaka 2020, ufyatuaji wa risasi bila kukusudia na watoto walio na umri wa chini ya miaka 18 ulisababisha vifo vya watu 142 na 242 kujeruhiwa.
Mnamo mwaka wa 2021, idadi ya vifo ilipanda hadi 154 na idadi ya watu waliojeruhiwa iliongezeka kidogo hadi 244. Na, kwa mujibu wa kundi hilo, watu 16 wameuawa na 29 wamejeruhiwa katika risasi hizi hadi sasa mwaka huu.
Kulingana na ripoti ya 2021 iliyokagua kipindi cha miaka sita kinachoisha mnamo 2020, kikundi hicho kilipendekeza sababu kadhaa zimechangia ongezeko kubwa la ufyatuaji risasi katika miaka ya hivi karibuni.
Wakati vijana wenye umri wa kati ya miaka 14 na 17 walichangia zaidi ya matukio haya ambapo walijipiga risasi wenyewe au mtu mwingine kwa bahati mbaya - 776 - katika kipindi hicho cha miaka sita, watoto wa umri wa miaka mitano au chini walichangia jumla ya pili ya 610.