Breaking

Saturday, 12 March 2022

KAMATI KUU CCM YAITAKA SERIKALI KUCHUNGUZA MWENENDO WA JESHI LA POLISI



Na Samir Salum  - Lango la habari 

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana jana Dodoma, chini ya Mwenyekiti wake Samia Suluhu, imeiagiza Serikali kuchunguza mwenendo wa Jeshi la Polisi baada ya wananchi kupoteza imani na Jeshi hilo.


Taarifa hiyo imetolewa leo Machi 12, 2022, na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka, jijini Dar es Salaam.


Shaka amesema kuwa baadhi ya Maofisa wa Polisi hawaaminiki na wanaonekana kutenda majukumu yao bila kufuata Mwongozo wao wa kisheria (PGO)


"Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, imeielekeza serikali kuangalia upya mwenendo wa jeshi la polisi nchini ambao umekuwa ukilalamikiwa na wananchi kutokana na matendo yanayofanywa na baadhi ya maafisa kinyume na miongozo ya utendaji wa kazi," amesema Shaka


Aidha amesema kuwa kamati hiyo imempongeza Rais Samia kwa hatua alizozichukua kufuatia mauaji yaliyofanyika mkoani Mtwara na Tanga.


.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages