Breaking

Tuesday, 8 March 2022

JAMII YATAKIWA KUWA NA UTAYARI WA KUTOA TAARIFA ZA UKATILI WA KIJINSIA

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha

**********

Jamii imetakiwa kuwa tayari kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia katika jamii ikiwemo ukeketaji kwa watoto wa kike ili kuleta usawa.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju wakati akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.

Mpanju amesema kuwa ni vyema jamii ikapambana na vitendo vya ukatili hasa dhidi ya Wanawake ili kutorudisha nyuma juhudi za Serikali na wadau za kuleta Usawa wa kijinsia.

Amesema jamii inatakiwa kusimama katika kupambana na kupinga Mila hasi za kumnyima mwanamke haki na kumkandamiza katika kupata fursa mbalimbali zinazojitokeza kwenye jamii ili kumuwezesha mwanamke kuwa na uwezo wa kutatua changamoto zinazomkabili.

Kwa upande mwingine Mpanju amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya mapinduzi makubwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake kwa kuwezesha wanawake kufikia kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu.

Amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia kumefanyika mapinduzi makubwa na hatua kubwa imepigwa katika kujenga kizazi cha haki na usawa huku wanawake wakichaguliwa na kuteuliwa kuongoza Idara nyeti katika taifa.

“Wanawake ni nguzo ya maendeleo duniani. Ndani ya mwaka mmoja wa Uongozi wa Rais Samia tumepiga hatua kubwa ndani ya mwaka mmoja, tuna Rais Mwanamke, Spika wa Bunge Mwanamke, Katibu Mkuu wa Bunge mwanamke, tuna Mawaziri wanawake 9 katika Wizara nyeti wanafanya kazi vizuri na maendeleo tunayaona, mambo yanakwenda vizuri”,amesema Mpanju.

Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha kwa lengo la kuwakutanisha Wanawake na wadau wengine katika kujadili changamoto zinazowakabili Wanawake na Ustawi wao limeongozwa na kauli mbiu ‘Kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu, Tujitokeze kuhesabiwa’.



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkurugenzi wa TGNP Lilian Liundi (kulia) akifuatilia hotuba ya
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju wakati akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Wanachama wa TGNP, Gemma Akilimali (kushoto) na Jovitha Mlay wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Wanachama wa TGNP, Gemma Akilimali (kushoto) na Jovitha Mlay wakiwa kwenye Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akifungua Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika leo Jumatatu Machi 7,2022 Jijini Arusha.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages