Breaking

Monday, 14 March 2022

WATU WANNE WAFARIKI, 35 WAJERUHIWA AJALI YA BASI LA KILIMANJARO



Basi la kampuni ya Kilimanjaro EXPRESS linalofanya safari kutoka Tunduma kwenda Dar es Salaam limepata ajali maeneo ya Senjele mkoani Songwe.

Basi hilo limepata ajali leo Jumatatu Machi 14, 2022 asubuhi wakati likielekea Dar es Salaam.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Senjele ya Pili mkoani Songwe ambapo Kwa mujibu wa mashuhuda chanzo cha ajali inaelezwa kuwa dereva aliyejaribu ku-overtake katika mazingira ambayo hayaruhusu zoezi hilo na kupelekea gari hilo kuacha njia na kupinduka.



Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Rashid Ngonyani amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa  watu hao wanne wamefariki dunia papohapo na wengine 35 wakijeruhiwa.


Amesema kuwa majeruhi wamepelekwa hospitali kupata matibabu huku miili ya marehemu ikihifadhiwa katika hospitali ya Vwawa.


( Endelea kufuatilia Lango la habari kwa taarifa zaidi )




Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages