Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja linamshikilia YUNUS NASSOR ALI (32) kwa tuhuma za kujifanya afisa usalama wa Taifa.
Akithibitisha tukio hilo mbele ya waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Mjini Magharibi ACP. ABDALLAH MUSSA amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa mnamo tarehe Machi 11, 2022 majira ya saa 11:00 jioni huko Kilima Hewa wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo alihusika katika matukio mbalimbali ya wizi wa pikipiki aina ya Click pamoja na kujifanya Afisa Usalama wa Taifa.
Aidha baada ya kufanya upekuzi nyumbani kwake Kilima Hewa Wilaya ya Mjini alipatikana na nyaraka mbalimbali za Serikali.